Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA74

Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu  Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.

Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa China akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 74
UN Photo/Loey Felipe

Asilani hatutotiwa woga na vitisho:China

Katika hotuba yake kwenye mjadala Mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa Diwani wa jimbo na waziri wa mambo ya nje wa Uchina ametangaza kwamba nchi yake asilani haitotiwa woga na vitisho au kukubali shinikizo wakati inapokabiliwa na changamoto za ulinzi.