Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.
MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Mkutano wa Kiir na Machar umerejesha imani Sudan Kusini- Deng Gai
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limejulishwa kuwa mkutano kati ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na mpizani wake Riek Machar kwenye mji mkuu Juba hivi karibuni ulikuwa ni fursa pekee ya kutatua masuala muhimu ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kwenye mzozo unaoendelea nchini humo.
Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya aeleza Rais Uhuru Kenyatta
Tumefika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuungana na nchi wanachama kuelezea ambayo Kenya imeyafanya katika kuhakikisha inaendana na vipaumbele vya mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja huo UNGA74 ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ujumuishwaji na ushirikiano wa kuhakisha utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030.
Dunia inahitaji madini, ajira za viwandani, mafunzo na maendeleo- rais Tshisekedi
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC inauhitaji Ujumube wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO lakini inahitaji MONUSCO iliyo haraka kutekeleza wajibu wake, ulio na vifaa, ulio thabiti na ambao una wajibu sahihi, amesema rais wa DRC, Felix Tshisekedi katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Leo Alhamisi Septemba 26.
Ufadhili wa SDGs na mabadiliko ya tabianchi unademadema:UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya mbele ya mjadala mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba kuna pengo kubwa la ufadhili ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kukabiliana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.
Kutokomeza nyuklia ni kuachana nazo kabisa- Guterres
Njia pekee ya kutokomeza tishio la silaha za nyuklia duniani ni kuachana kabisa na silaha hizo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kando mwa mjadala mkuu wa baraza hilo jijini New York, Marekani.
Kenya tunasonga ingawa bado tuko mbali, asema Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema nchi yake inajitahidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na imepiga hatua ingawa bado kuna safari ndefu.
26 Septemba 2019
Wanawake wanahitajika zaidi katika tasnia ya ubaharia kama ilivyo tasnia nyingine, linasema shirika la kimataifa la shughuli za usafirishaji wa majini IMO. Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya asema Rais Uhuru Kenyatta. Na Profesa Antoine Kiamiantako Miyamueni, mdadhiri wa masuala ya uchumi katika chuo kikuu cha Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC) amesema ushirikiano baina ya vyuo vikuu utasaidia kuinua elimu Afrika.
Ushirikiano baina ya vyuo vikuu utasaidia kuinua elimu Afrika- Profesa Miyamueni
Jukwaa la kimataifa la vyuo vikuu barani Afrika na ughaibuni kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na mustakabali wa elimu katika bara hilo, limezinduliwa rasmi kwenye makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.
Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya:rais Kenyatta
Tumefika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuungana na nchi wanachama kuelezea ambayo Kenya imeyafanya katika kuhakikisha inaendana na vipaumbele vya mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja huo UNGA74 ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ujumuishwaji na ushirikiano wa kuhakisha utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030.
Pagination
- 1
- 2