Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.
MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Kenya tunasonga ingawa bado tuko mbali-Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema nchi yake inajitahidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na imepiga hatua ingawa bado kuna safari ndefu.
Ahadi ni deni: Mkutano wa kihistoria kutoa msukumo wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo.
Umoja wa Mataifa unasema uchumi endelevu wa dunia ule ambao unailinda dunia na kuboresha maisha ya kila mtu kila mahali ni fursa nzuri ya kuleta ajira na masoko yenye thamani ya matrilioni ya dola. Ili kutimiza hilo , jamii ya kimataifa inahitaji kuongeza kasi ya uwekezaji.
Tunaomba jamii ya kimataifa kwenda nasi bega kwa bega kutatua majanga CAR - rais Touadera
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Faustin Archange Touadera hii leo Jumatano ametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa, tofauti, unaoeleweka, na ulio na utaratibu katika kukabiliana na janga linalokabili nchi yake, akielezea msaada wa serikali kuendelea kusaidia raia wake kuibuka kutoka hali ya sasa.
Licha ya hatua zilizopigwa, safari bado ni ndefu kutimiza haki za mtoto- Katibu Mkuu
Tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za mtoto miaka 30 iliyopita pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kote duniani bado vita imesalia kuwa chanzo kubwa ya ukiukwaji wa haki za mtoto na bado kuna nchi hazijaridhia mkataba huo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
25 Septemba 2019
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awaeleza wajumbe wa mjadala wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuwa hatua zimepigwa lakini bado wana kazi katika kutimiza haki za mtoto.
Tumepiga hatua lakini bado tuna kazi katika kutimiza haki za mtoto:Guterres
Tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za mtoto miaka 30 iliyopita pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kote duniani bado vita imesalia kuwa chanzo kubwa ya ukiukwaji wa haki za mtoto na bado kuna nchi hazijaridhia mkataba huo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.