Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA74

Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu  Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.

Mtizamo wa Baraza Kuu wakati wa ufunguzi wa kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mwaka 2019. (Septemba 23, 2019)
UN Photo/Loey Felipe

Greta Thunberg ahoji uthubutu wa viongozi kusalia na maneno huku watu wakipoteza maisha

Leo katika ufunguzi wa  mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutrerres amesema hatakuwa mtamazaji aliye kimya kwa uhalifu ambao unaathiri hali ya sasa na  kuharibu haki kwa vizazi vijavyo kwa ajili ya mustakabali endelevu akiongeza kwamba viongozi wana haki ya kufanya kila wawezalo kukomesha janga la mabadiliko ya tabianchi kabla halijatukomesha.

23 Septemba 2019

Miongoni mwa atakayokuletea Grace Kaneiya kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa

-Bila kutimiza huduma za afya na za msingi kwa jamii zote duniani utekelezaji wa SDGs waninekana kama ndoto kwa mujibu wa WHO na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

-Nchini Uganda wanaichi wanena kuhusu changamoto za huduma za afya

-Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya tabia nchi ni sasa kunusuru kizazi kilichopo na kijacho wasema Umoja wa mataifa kwenye mkutano dhidi ya tabianchi

Sauti
11'56"
Mkulima karibu na mji wa Kisumu nchini Kenya akilima shamba lake.
World Bank/Peter Kapuscinski

Lengo langu ni kuona vijana wanashiriki kilimo chenye tija na si bora kilimo - Mugo

Viongozi wa dunia wakikutana leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New  York Marekani kupitia azimio la kusongesha hatua kwa tabianchi, nchini Kenya vijana hivi sasa wanashiriki katika kilimo si tu chenye kuwawezesha kupata kipato bali pia kile kinacholinda na kuhifadhi mazingira lakini wanataka msaada zaidi ili waweze kusonga mbele.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Adhanom Ghebreyesus alipozuru Butembo nchini DRC Aprili mwaka 2019 baada ya watu wenye silaha kushambulia kituo cha Ebola
WHO/Junior Kannah

Nchi ziwekeze asilimia 1 katika huduma za afya kwa wote, WHO

Nchi ni lazima ziongeze matumizi kwenye huduma za kimsingi za afya kwa takriban asiliamia 1 ya pato loa la kitaifa ikiwa dunia inataka kupunguza mianya ya kutimiza malengo ya afya ifikapo mwaka 2015,  kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani na washirika kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa huduma za afya zilizo muhimu.