Mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 25 septemba 2018 hadi Oktoba mosi 2018. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Kifua Kikuu, Ulinzi wa Amani, tukio maalum la kumuenzi hayati Nelson Mandela na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.
MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Imani imetoweka duniani, ushirikiano wa kimataifa nao mashakani- Kenya
Ongezeko la uelewa wa wananchi kuhusu rasilimali zilizopo na huduma wanazopata kutoka kwenye serikali zao ni moja ya mambo yaliyotajwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuwa yanasababisha wananchi kukosa imani na taasisi zao zinazowaongoza.
Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa ugonjwa wa Kifua Kikuu ndio unaongoza kwa kuwa ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza duniani. Takwimu za hivi karibuni zaidi za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa hivi sasa watu milioni 10.4 duniani kote wameambukizwa ugonjwa huo huku milioni 1.6 wakifariki dunia kila mwaka. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la afya .WHO linataka mbinu mtambuka za kuondokana na ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030. Miongoni mwa mbinu hizo ni kutumia manusura wa ugonjwa huo kama wajumbe wa kuelimisha jamii ili ijikinge au isake tiba.
Hatua kali ni lazima katika kuzuia kuenea silaha za maangamizi-SC
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametaka mshikamano na hatua kali kutoka kwa baraza hilo dhidi ya silaha za maangamizi zikiwemo za nyuklia, kibaolojia na za kemikali.
Uchaguzi utafanyika mwaka huu DRC kama ilivyopangwa:Kabila
Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu hautobadilishwa utafanyika kama ilivyopangwa.
Afrika tumieni fursa ya biashara huru kukuza viwanda na uchumi:UNIDO
Katika miongo michache ijayo Afrika imeelezwa itakuwa bara changa na lenye watu wengi zaidi duniani , huku idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi ikitarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 450 sawa na asilimia 70 ifikapo mwaka 2030.
Bado haki za binadamu zimesalia ndoto kwa wakazi wengi duniani- UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema miaka ya 70 ya tamko la haki za binadamu duniani, haijawa tiketi kwa kila mtu kufarahia haki za msingi zilizoainishwa katika nyaraka hiyo.
Kutobaini mapema na kutibiwa TB ni mtihani mkubwa Afrika:WHO
Fursa ya kutopimwa mapema, kugundulika na kupata matibabu yanayostahili ya ugonjwa wa kifua kikuu ndio mtihani mkubwa wa mapambano ya vita dhidi ya ugonjwa huo barani Afrika.