Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

UN Picha/Greg Kinch

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Ibara ya 23 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi anayoifanya, kufanya kazi katika mazingira salama na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira. Kipengele cha pili kwenye ibara hiyo kinasema kuwa kila mtu, bila kubaguliwa ana haki ya kulipwa mshahara sawa kwa kazi sawa. Ibara hiyo inakwenda mbali zaidi na kusema kuwa kila mtu ana haki ya ujira unaofaa kwa ajili ya matumizi yake na familia kuwawezesha kuishi kwa utu na nyongeza kwa ajili ya ulinzi wa kijamii.

Sauti
5'14"