Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa, jinsia, lugha, dini, siasa, fikra, asili ya taifa la mtu, miliki , kuzailiwa au kwa hali nyingine yoyote.

Halikadhalika hakuna ubaguzi utakaotendwa kwa misingi ya kisiasa, kimamlaka au hadhi ya kimataifa ya nchi au utawala ambao mtu fulani anatoka, iwe ni huru, iwe chini ya  udhamini, isiyojitawala au chini ya mazingira mengine yenye udhibiti wa kimamlaka.

Sauti
52"