Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNHCR/Rocco Nuri

Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19  

Kufuatia mlipuko wa COVID-19 mnamo Machi mwaka huu nchini Uganda, shule zilifungwa na hivyo kuwaweka hatarini watoto kukumbana na ukatili wa kijinsia hasa katika makazi ya wakimbizi ambako huduma nyingi huwa hazitoshelezi jamii hizo. Kwa mantiki hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa kupitia wadau wake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuhamasisha jamii kuhakikisha ulinzi wa watoto wa kike na wale wa kiume. Sasa, watoto wenyewe wanashirikishwa katika kampeni ya kuwalinda kwa kuwapatia nafasi ya kuzungumzia changamoto na mikakati ya kuzikabili. 

Sauti
3'29"