Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

 “Unyanyapaa husababisha habari potofu na ubaguzi. Hiyo inatuzuia kusonga mbele. " Clara, 23, Hispania
© UNICEF/@witchtropolis

Uzoefu wa UNAIDS katika VVU/UKIMWI watoa mwongozo wa kupunguza unyanyapaa wakati wa COVID-19 

Kwa kutumia uzoefu wake wa miaka 40 ya kushughulikia ugonjwa wa UKIMWI, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI, UNAIDS, limetoa mwongozo mpya kuhusu jinsi ya kupunguza unyanyanyapaa na ubaguzi wakati wa kushughulikia COVID-19. Mwongozo huo unategemea ushahidi wa hivi karibuni juu ya kile kinachofanya kazi kupunguza unyanyapaa na ubaguzi unaohusiana na Virusi Vya UKIMWI, VVU na unatumika kwa COVID-19. 

Matumizi ya mtandao kupitia simu ya rununu
Unsplash/Priscilla du Preez

COVID-19 yashamirisha biashara mtandaoni:UNCTAD 

Janga la corona au COVID-19 limebadili mtazamo wa watu kuhusu kuelekea zaidi kwenye ulimwengu wa kidijitali kwa mujibu wa matokeo ya utafidi wa wateja uliofanywa hivi karibuni ya shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD.