Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Nchini Niger, mashambulio dhidi ya raia na vikundi visivyo vya serikali na operesheni za kijeshi zimekuwa zikiongezeka, na kufungwa kwa mipaka na hatua zingine za kuzuia COVID-19 zimesababisha maalum yaliyoko hatarini kuathirika.
© UNICEF/Juan Haro

Nchi 1 kati ya 8 ndio zenye mipango ya kulinda wanawake dhidi ya athari za COVID-19: UN 

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na lile la mpango wa maendeleo UNDP kuhusu hatua za kimataifa za kukabiliana na janga la corona au COVID-19 katika suala la kijinsia zinaonyesha kwamba mikakati ya hifadhi ya jamii na masuala ya ajira wakati wa janga hili imeyapa kisogo mahitaji ya wanawake.