Skip to main content

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN Kenya/Newton Kanhema

COVID-19 imenirudisha nyumbani kijijini-Waweru

Tangu lizuke janga la corona duniani athari nyingi za karibu kila sekta zimeshuhudiwa. Vijana ambao idadi yao ndiyo kubwa kwa karibu kila nchini duniani nao wameathirika pakubwa. Wengi walilazimika kusitisha masomo kufuatia kufungwa shule na taasisi za elimu, wengine wakapoteza ajira na kubaki katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya maisha yao. Kijana Joseph Waweru alipoteza kibarua chake mjini Nairobi na pia mipango yake ya masomo katika chuo kikuu ikakwama ndipo akaamua kuhamia kwao alikozaliwa huko Kitale, magharibi mwa Kenya.

Sauti
3'35"
UNICEF VIDEO

Nilipokuwa nakua, ukatili majumbani niliona jambo la kawaida, sasa hapana!

Livhuwani Hellen Dzibana, mshauri nasaha kutoka nchini Afrika Kusini, kutwa kucha hivi sasa anaomba janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 limalizike kwa kuwa limekuwa mwiba katika utekelezaji wa majukumu yake kwa ufasaha ya kusaidia manusura wa ukatili wa kingono, jambo ambalo analisimamia kidete baada ya kulitambua kwa kina. Kulikoni? 

Livhuwani, mkazi huyu wa mji mkuu wa kibiashara wa Afrika Kusini, Johannesburg anasema kwamba katu wakati wa makuzi yake hakuwahi kufahamu maana ya ukatili wa kijinsia.

Sauti
2'5"

16 Septemba 2020

COVID-19 ni zaidi ya janga la kiafya ni mzahma ya kibinadamu. Mshauri nasaha Afrika Kusini alalama COVID-19 kukwamisha kazi yake. Vita iliniondoa chuo kikuu kwetu Yemen, watu wa Jordan wamenipa fursa nyingine-Mkimbizi.

Sauti
12'48"
Timu ya wanasayansi katika taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford na Kundi la chanjo la Oxford wanaendelea na utafiti kugundua chanjo salama, yenye ufanisi dhidi ya virusi vya corona.
University of Oxford/John Cairns

COVID-19 ni zaidi ya janga la kiafya, ni zahma ya kibinadamu:UN 

Akizindua ripoti hiyo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “hakuna nchi ambayo imenusurika, hakuna kundi la watu ambalo halijaguswa na gonjwa hilo na hakuna mtu aliye na kinga dhidi ya athari za janga hilo.” 

Sauti
2'35"
Livhuwani Hellen Dzibana, (kulia) akizungumza na moja ya wateja wake jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
UNICEF VIDEO

Wakati nakua, ukatili majumbani niliona jambo la kawaida, sasa hapana!

Livhuwani Hellen Dzibana, mshauri nasaha kutoka nchini Afrika Kusini, kutwa kucha hivi sasa anaomba janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 limalizike kwa kuwa limekuwa mwiba katika utekelezaji wa majukumu yake kwa ufasaha ya kusaidia manusura wa ukatili wa kingono, jambo ambalo analisimamia kidete baada ya kulitambua kwa kina. Kulikoni? 
 

Sauti
2'5"