Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNICEF/UNI315623/Ongoro

Redio 500 za sola zatolewa na UNMISS kusaidia watoto kusoma wakati huu wa COVID-19

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umegawa redio 500 zinazotumia sola kwa jamii za Yambio , jimbo la Equatoria Magharibi ili kuwasaidia watoto waliosalia majumbani kutokana na janga la corona au COVID-19 kuweza kusoma. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Katika moja ya vijiji vya Yambio watoto wakiwa wamekusanyika nje pamoja wakisikiliza masomo kwa njia ya Redio ambazo zimesambazwa na UNMISS.

Sauti
2'35"