Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

1 SEPTEMBA 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema muhula mpya wa masomo ukianza Agosti hadi Oktoba mwaka huu, theluthi moja ya wanafunzi bilioni 1 nukta 5 wa shule za awali hadi sekondari ndio wamejiandaa kurejea shuleni.Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na wadau wamekarabati na kukabidhi vyumba 16 vya huduma za dharura kwa ajili ya janga la corona au COVID-19 kwenye kituo cha wagonjwa mahututi mjini Yambio Magharibi mwa jimbo la Equatoria.  Mwalimu mkimbizi ahofia kuwa fursa a

Sauti
12'24"