Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN /Manuel Elias

Mipango ya kudhibiti COVID-19 ilianza punde tu baada ya maambukizi kuripotiwa China, yasema Mauritius

Mauritius, taifa la kisiwani lililo katika bahari ya Hindi limeelezea kile kilicholiwezesha kudhibiti ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 punde tu baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa wagonjwa 3 nchini humo. Ahimidiwe John Kibego na maelezo zaidi. 

Fukwe katika mji mkuu wa Mauritius, Port Louis, zikionekana tupu bila wageni wowote wakati wa zama za mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 mwezi Machi mwaka  huu wa 2020. 

Sauti
2'23"