Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN News/ John Kibego

Kwa sasa nimewaambia wakimbizi wenzangu tusishikane mikono, tusitembeleane- Acces Bazibuha  

Sasa ni makala ambapo tunafuatilia hali ilivyo na mikakati inayowekwa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la afya WHO na wizara ya afya ya nchini hiyo kuzuia kuenea kwa COVID-19 kufuatia mlipuko wake katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kusababisha kifo cha mkimbizi mmoja hapo tarehe nane Agosti mwaka huu. Moja ya hatua ilikuwa ni kuzuia watu kutembea huku na kule, na pia kufuatilia watu waliokutana na mkimbizi aliyeambukizwa. 

Sauti
54"
MINUSCA/Screenshot

Kwa wasiojua kusoma, michoro kwenye kuta CAR ni jawabu katika kujikinga na COVID-19

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, MINUSCA umeshirikiana na serikali kuchora picha za kuelimisha watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ambao hadi sasa nchini humo umesababisha vifo vya watu 61 miongoni mwa wagonjwa 4,652 waliothibitishwa. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.

Michoro hiyo katika mji mkuu wa CAR, Bangui pamoja na kuonesha dalili za COVID-19, pia inaonesha unyanyapaa na mbinu za kujikinga.

Sauti
1'56"
© UNICEF/Andrea Campeanu

UNICEF yasema kuendeleza huduma za msingi Sudan Kusini ni muhimu katika mapambano ya COVID-19

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema muendelezo wa huduma za msingi zikiwemo chanjo kwa watoto Sudan Kusini ni muhimu sana katika vita dhidi ya janga la corona au COVID-19 na maradhi mengine. Loise Wairimu na taarifa zaidi.

Kwa mujibu wa UNICEF, nchini  Sudan Kusini asilimia 60 ya watu wanakosa huduma ya maji safi, watoto milioni 1.3 wataugua utapiamlo na kiwango cha chanjo hivi sasa ni asilimia 40 tu.  

Sauti
1'53"

17 AGOSTI 2020

Katika Jarida la habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Janga la corona au COVID-19 labadili tabia za wananchi wa Lamu Kenya utamsikia muasisi na mkurugeni wa shirika lisilo la kiserikali la Safari Doctors Umra Omar akifafanua

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema ni muhimu kuendelea na huduma za msingi ikiwemo chanjo Sudan Kusini ili kukabili COVID-19

-Huko nchini CAR mpango wa Umoja wa Mataifa MINUSCA washirikiana na serikali kulimisha jamii kuhusu COVID-19 kwa kutumia michoro na picha

Sauti
11'3"