Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Wizara ya Afya ya Bogotá imetuma muuguzi kwenda katika eneo la Suba, kaskazini mwa Bogotá , Colombia kuwahudumia watu wa jamii za asili.
PAHO/Karen González Abril

COVID-19 imekuwa na athari mbaya kwa zaidi ya watu wa asili milioni 476 kote ulimwenguni. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa njia ya video kuhusu siku ya leo ya watu wa asili ambayo huadhimishwa Agosti 9 ya kila mwaka, amesema  ni muhimu kwa nchi kuandaa rasilimali ili kushughulikia mahitaji ya watu wa asili, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao kujibu mahitaji yao, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao zisizopingika.