Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN News

COVID-19 imeongeza chumvi katika kidonda changu cha athari za mabadiliko ya tabianchi-Jemima Hosea 

Kutokana na mwamko wa watu nchini Tanzania kuyapenda mazingira ya nyumba zao, Jemima Hosea wa jijini Dar es Salaam, aliona hiyo ni fursa ya yeye kujipatia kipato kwa kuotesha na kuuza maua ya aina mbalimbali. Katika kipindi ambacho biashara yake ilikuwa imeanza kushamiri ndipo likaibuka janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. Janga hili likaongeza machungu katika changamoto aliyokuwa anapambana nayo mfanyabiashara huyu-changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa amemtembelea Jemima na kutuandalia makala hii. 

Sauti
2'49"

20 July 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo.

-  Shirika la afya ya wanyama duniani OIE na shrika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO leo wamezindua mkakati wa pamoja wa hatua za kimataifa za kuzuia kusambaa kwa homa ya mafua ya nguruwe ya Afrika

-  Mkimbizi raia wa Syria ambaye hivi sasa anaishi Ufaransa, amejizolea sifa kwa kuandaa chakula kwa ajili ya kuwasambazia wafanyakazi walioko katika mstari wa mbele wa kupambana na janga la COVID-19 katika nchi yake mpya.
- Sintosahau nilichokishuhudia kambini Bangladesh:Mkimbizi Asma 

Sauti
9'55"