Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Jason Nyakundi

Nimevumbua kifaa cha kumsaidia mgonjwa kupumua akiwa njiani kwenda Hospitali

Wakati nchi nyingi zikijaribu kupambana na janga la virusi vya corona au COVID-19 kwa kuwahudumia wagonjwa wanaoongezeka kila uchao, wito pia unatolewa kwa watu wote kila mtu kwa namna ifaayo, kuchangia katika vita hii. Mmoja wa watu walioitikia wito huo ni kijana Peter Mbiria ambaye amefanikiwa kuunda kifaa cha kuwasaidia wagonjwa kupumua ambacho zaidi kinaweza kutumiwa kutumiwa kusambaza hewa wakati mgonjwa yuko kwenye gari la kubeba wagonjwa akisafirishwa kwenda hospitalini. Ungana na Jason Nyakundi katika mahojiano haya.

Sauti
5'12"

15 Julai 2020

Hii leo tunamulika janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa muktadha mbalimbali ambapo UNICEF inasema suala la maji kwenye janga hili si la uhai tu bali pia ni lazima. IOM nayo inasema wahamiaji si wasambaza virusi bali wako mstari wa mbele kutoa huduma katikati ya janga hili. Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la mitaji ya maendeleo, UNCDF limesaidia kuchochea maendeleo kwenye halmashauri ya mji wa Kibaha mkoani Pwani na makala tunamulika ubunifu wa kifaa cha kusaidia mgonjwa wa COVID-19 kupumua wakati akipelekwa hospitali, na hii ni kutoka Kenya.

Sauti
11'21"