Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN Women /Aidah Nanyonjo

Mimi kama mbunge ni wajibu wangu kuielimisha jamii jinsi ya kujikinga na COVID-19-Mbunge David Karubanga wa Uganda

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo mchango muhimu wa mabunge na wabunge unatambuliwa katika kuwawakilisha wananchi na kupaza sauti zao ili serikali imweke mwanajamii katika katika vipaumbele vyake inapoweka mipango ya nchi. Katika zama hizi za COVID-19, mabunge na taasisi nyingine za serikali nazo zimelazimika kwa kiasi fulani kufuata utaratibu mpya kujikinga na virusi ikiwemo kuweka umbali kati ya mtu na mtu na hata wakati mwingine kulazimika kufanya kazi nje ya majengo ya bunge kama ilivyo kawaida.

Sauti
3'39"