Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19
UN Photo/Evan Schneider

Nchi 30 na wadau wa kimataifa wajiunga kupiga jeki C-TAP:WHO

Nchi 30 na wadau mbalimbali wa kimataifa na taasisi wamejiunga kusaidia mkakati wa fursa za kiteknlojia dhidi ya janga la virusi vya corona au COVID-19 ujulikanao kama C-TAP, mkakati wenye lengo la kufanya chanjo, vipimo, matibabu na teknolojia zingine za kupambana na COVID-19 kupatikana kwa kila mtu, kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.