Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Kala Jeremiah anayesifika kwa nyimbo za kijamii, sasa aja na CORONA IPO.

Wakati mapambano dhidi ya virusi vya corona yakiendelea duniani kote, wito umekuwa ukitolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuwa ni jukumu la kila mtu kuwalinda wengine kama anavyojilinda hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu namna bora za kujilinda ambaz

Sauti -
3'57"

Vita dhidi ya COVID-19 na utimizaji wa SDGs ni mitihani inayohitaji fedha:UN

Mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo umefanyika leo Alhamisi ukihusisha Umoja wa Mataifa  na maafisa wawakilishi wa serikali mbalimbali, lengo kubwa likiwa ni kuchagiza msaada wa kimataifa wa fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zimedhoofishwa Zaidi na mlipuko wa janga la virusi vya corona au COVID-19 katika katika hatua zake za utumizaji wa malengo ya maendeleo endelevu , SDGs.

28 Mei 2020

-Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa :

-Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM  la sema tushikamane kuchangia na kuwanusuru Wasyria na  COVID-19

- Kuelekea siku ya walinda amani duniani kesho Mei 29, tunamulika askari wanawake wa Tanzania.

Sauti -
13'21"

Kutana na Sajini Desta anayesifika kwa kutengeneza magari ya UNMISS, Sudan Kusini

Wanawake wanaohudumu katika shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote duniani wanaendelea kujizolea umaarufu kutokana na uchapakazi wao. Mmoja wao ni Almaz Kabtimer Desta, Sajenti anayefanya kazi katika Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNIMISS akihudumu kama fundi makenika.

Chonde chonde tushikamane kuchangia na kuwanusuru Wasyria na COVID-19:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema fedha za ufadhili kwa ajili ya maelfu ya raia wa Syria waliotawanywa na machafuko inasalia kuwa kipaumbele kinachotia hofu kubwa ya utoaji msaada wa kibinadamu hasa wakati huu ambapo janga la virusi vya corona au COVID-19 linaongeza msumari wa moto juu ya kidonda.