Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

WFP/Mahamady Ouedraogo

WFP yaendelea kunusuru wahitaji, katikati ya COVID-19,

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP, linaendelea kusaka rasilimali ili liweze kufikisha misaada kwa watu milioni 100 kwa mwaka huu 2020. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Misaada hiyo ikiwemo ya chakula ni muhimu kwa jamii zilizo hatarini ambapo WFP inasema kuwa kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii ni muhimu ili watu wengine milioni 130 wasitumbukie kwenye njaa kutokana na janga la virusi vya Corona au COVID-19.

Sauti
1'55"

13 Mei 2020

Kampeni ya #Reimagine kuibuka na mpango wa dunia ya watoto baada ya COVID-19. Kitengo cha damu salama katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kimewatoa hofu wachangiaji wa damu kuwa uwepo wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 usiwatishe kwenda kuchangia damu. Katikati ya COVID-19, WFP yaendelea kunusuru wahitaji.

Sauti
12'11"