Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Machifu watumiwa Niger kuhamasisha dhidi ya COVID-19
Kwenye kitongoji cha Banizoumbou katika mji mkuu wa Niger, Niamey, Chifu Yaye Modi Alzouma, anahamasisha wananchi juu ya virusi vya Corona, akisema kuwa hata machifu wamekiri kuwepo kwa gonjwa hilo.
Hatua hii ya Chifu Alzouma ni sehemu ya kampeni zinazoendeshwa kwa ushirikiano na UNICEF zikijumuisha viongozi wa jadi na wapiga debe mjini Niamey.
Kampeni inalenga kuhamasisha jamii ielewa COVID-19, na izingatie kanuni za kutochangamana, na kuheshimu amri ya dharura ya kutotembea hovyo.
Madawa ya kulevya yapanda bei, kisa? COVID-19
Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, UNODC imesema janga la virusi vya corona au COVID-19 limeathiri utaratibu wa usafirishaji haramu wa mihadarati hususan kwa njia ya anga na hivyo kuwafanya wasafirishaji haramu kusaka njia mbadala. Jason Nyakundi na taarifa zaidi
07 MEI 2020
Katika Jarifda la Habari hii leo kwenye Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lasema takribani watoto milioni 116 watazaliwa wiki 40 baada ya kutangazwa rasmi kuwa janga la corona limekuwa janga la kimataifa mnano mwezi Machi makwa huu
- Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC imesema janga la COVID-19 limeingilia utaratibu wa kusafirisha mihadarati kwa njia ya anga na kuwafanya wafanyabiashara wa bidhaa hizo haramu kusaka njia mbadala
UN yatoa ombi la dola bilioni 6.7 kulinda mamilioni ya watu dhidi ya COVID-19 katika nchi masikini
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA ametoa wito wa kuchukuliwa hatua Madhubuti ili kuepuka athari kubwa za mlipuko wa janga la corona au COVID-19 wakati akitoa ombi la dola bilioni 6.7 huku akieleza mipango ya kimataifa ya kupambana na virusi vya corona katika nchi zisizojiweza.
Machifu Niger wapita mtaa kwa mtaa kuelimisha watu kuhusu COVID-19
Nchini Niger, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na viongozi wa kijadi kusaidia kuelimisha jamii ijikinge dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, katika taifa hilo ambako tayari kuna wagonjwa 763 na kati yao hao, 38 wamefariki dunia. Maelezo zaidi na Loise Wairimu.
COVID-19 inabadili mfumo wa usafirishaji haramu wa mihadarati :UNODC Ripoti
Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, UNODC imesema janga la virusi vya corona au COVID-19 limeathiri utaratibu wa usafirishaji haramu wa mihadarati hususan kwa njia ya anga na hivyo kuwafanya wasafirishaji haramu kusaka njia mbadala.
Watoto milioni 116 kuzaliwa miezi 9 baada ya COVID-19 kutangazwa janga, je changamoto ni zipi?
Kuelekea siku ya mama duniani tarehe 10 mwezi huu wa Oktoba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linakadiria kuwa watoto milioni 116 watakuwa wamezaliwa wiki 40 tangu ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 utangazwe kuwa janga la kimataifa tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu.