Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

29 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula WFP yataka serikali kuchukua hatua kuepusha janga la njaa hasa baada ya watoto milioni 370 kukosa mlo shuleni kutokana na janga la virusi vya corona au COVID-19

-Kambini Dadaab nchini Kenya waalimu watumia Radio kutoa elimu kwa maelfu ya watoto waliolazimika kusalia nyumbani kutokana na janga la corona

Sauti
11'40"