Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNFPA yatarajia ongezeko la kesi za mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia zitakazo tokana na janga hili la COVID-19
© UNFPA Myanmar/Yenny Gamming

Mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji mwingine wa kijinsia huenda vikaongezeka wakati janga la COVID-19 linapoendelea-UNFPA

Wakati janga la COVID-19 likiendelea, idadi ya wanawake ambao hawawezi kupata upangaji wa uzazi, wanakabiliwa na ujauzito usiopangwa, ukatili wa kijinsia na mazoea mengine mabaya yanaweza kuongezeka kwa mamilioni katika miezi ijayo, kulingana na takwimu ziliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA.

Niger inakumbana na upungufu wa chakula na viwango vya mapato ya chini
WFP/Simon Pierre Diouf

COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi vyahitaji ujasiri na utashi kuvishinda:UN

Ili kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 na tishio linguine linalonyemelea la mabadiliko ya tabianchi njia pekee ya kukabiliana nayo ni “ujasiri, maono na uongozi wa ushirikiano, ukijikita katika mshikamano wa kimataifa amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa majadiliano ya kimataifa hii leo yaliyojikita katika mabadiliko ya tabianchi.

28 APRILI 2020

Katika jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Shirika la kazi duniani ILO leo likiadhimisha siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini limetaka waajiri kuwalinda wafanyakazi wakati na baada ya janga la virusi vya corona au COVID-19

- Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waliopona ugonjwa wa Corona waiasa jamii kuzingatia wito na masharti ya afya ili kujikinga na gonjwa hilo hatari

Sauti
12'12"