Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNICEF/Frank Dejongh

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Suala la unyanyapaa wa aina yoyote ile ni mtihani mkubwa katika jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao hutoa wito kila uchao kuhakikisha changamoto hiyo inatokomezwa .Wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 unyanyapaa umeelezwa kujitokeza na kusababisha changamoto kwa wagonjwa na washukiwa na hata kuwafanya wengine kutojitokeza kufanya vipimo hali ambayo shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kuwa ni hatari kubwa na kikwazo cha kupambana na ugonjwa huo.

Sauti
6'25"

24 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

-Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatiwa hofu na kamatakamata na kubanwa kwa vyombo vya habari wakati huu wa janga la COVID-19 ambapo taarifa sahihi ni muhimu sana

Sauti
10'46"