Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Nchini Uganda na Afrika Kusini, UN yazindua ombi la ufadhili kupambana na COVID-19
Nchini Uganda, ambako kuna wagonjwa 56 wa COVID-19, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Rosa Malango hii leo amezindua ombi la dharura la dola milioni 316 za Marekani kwa ajili ya kushughulikia janga hili.
Haki za binadamu ziwe muongozo wa vita dhidi ya COVID-19:UN
Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba haki za binadamu zinapaswa kuwa muongozo katika hatua zinazochukuliwa kupambana na janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19.
23 APRILI 2020
Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
Umoja wa Mataifa wasema teknolojia ya mawasiliano imedhihirisha umuhimu wake hasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 na hivyo kuhimiza wasichana wengi wawezeshwe kuingia katika teknolojia hiyo ya ICT
-Vifaa na misaada kutoka kituo kikuu kilichopo Addis Ababa Ethiopia vyaleta mabadiliko kwa maelfu ya watu katika vita dhidi ya COVID-19 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP
COVID-19 imedhihirisha umuhimu wa ICT duniani:Guterres
Janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID -19 limedhihirisha umuhimu wa teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA au ICT kwa wasichana na dunia nzima umesema Umoja wa Mataifa.