Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

OCHA/Franck Kuwonu

Tutahakikisha wakimbizi wako salama dhidi ya COVID-19 :UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linafanya kila juhudi kuhakikisha linanusuru maisha ya mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Magharibi na Kati yaliyo hatarini kutokana na changamoto mpya iliyozuka ya virusi vya Corona au COVID-19.

Shirika hilo linasema nchi 21 za kanda hiyo ambazo nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita, wakimbizi na wakimbizi wa ndani zinahitaji msaada ili kukabiliana na janga jipya linaloitikisa dunia hivi sasa.

Sauti
2'23"

20 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora ucha kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea

- Serikali ya Tanzania yaitikia wito wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO na leo imezindua mkakati wa ufundishaji kupitia teknolojia ya Radio na Televisheni kuhakikisha watoto wanasoma wakati huu wa COVID-19

- Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD Idris Elba na mkewe sabrina Elba leo wamezindua mfuko na ombi la dola milioni 200 kuwasaidia wakulima vijijini wakati huu wa janga la Corona ili kuhakikisha uhakika wa chakula

Sauti
13'24"