Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Shirika la afya Duniani WHO na Global Citzen kufanya tamasha la Muziki likimuhisha Lady Gaga pichani katika kuunga mkono na kuwasaidia wahudumu wa afya dhidi ya COVID-19
WHO

Tamasha la Dunia moja, pamoja nyumbani kufanyika leo:WHO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHODkt. Tedros Ghebreyesus na mawanamuziki nyota duniani Lady Gaga Pamoja na Hugh Evans kutoka mradi wa raia wa kimataifa au Global Citizen Ijumaa wametangaza kwamba “ wanamuziki wengi mashuhuru duniani , wasanii wa vichekesho na wahudumu wa kibinadamu watashiriki katika tamasha maalum la kimataifa mtandaoni lijulikanalo kama “One Worl, Together at Home “ likimaanisha dunia moja, wote kwa pamoja majumbani litakalofanyika hii leo.