Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Wafanyakazi wa afya ni askari wa mstari wa mbele dhidi ya COVID-19, tuwalinde
Askari wengi wameona vitisho vya vita kwa haraka, na ingawa ilikuwa ya kutisha mara nyingi, walijua ni nani wanapigana naye, na wangeweza kumtambua adui wao.
Andiko la Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe na Siddharth Chatterjee, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya.
COVID-19 imeumbua nchi tajiri na maskini- ILO
Shirika la kazi duniani, ILO limesema kuwa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, limeweka hadharani udhaifu wa masoko ya ajira duniani.
UN yawajulisha nchi wanachama kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19
Katika mkutano maalum kupitia njia ya mtandao uliofanyika leo Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo, Baraza la Usalama na baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC wamezijulisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu juhudi za Umoja huo katika kupambana na virusi vipya vya Corona, COVID-19 na kuendelea na kazi muhimu ya shirika hilo duniani kote.
ITU na UNESCO washirikiana kuhakikisha elimu kwa wanafunzi
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limezindua muungano wa elimu wa kimataifa ili kuhakikisha wanafunzi walio nje ya shule kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 wanasoma kupitia teknolojia. John Kibego na taarifa zaidi
(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)
Mlipuko wa COVID-19 unaathiri uwasilishaji wa mlo shuleni-WFP
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limezindua ramani mpya ya kidijitali inayodhihirisha athari za virusi vya Corona, COVID-19 katika program zake za mlo mashuleni. Flora Nduicha na taarifa kamili
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Kwa mujibu wa WFP ramani hiyo ambayo ni ya “ufuatiliaji wa kimataifa wa mlo mashuleni wakati wa kufungwa shule kutokana na mlipuko wa COVID-19 inatoa inatoa maenedeleo mapya ya kila siku kuhusu kufungwa kwa shule na idadi ya Watoto ambao hawapati tena mlo mashuleni kutokana na janga hili la Corona.
Mapambano dhidi ya COVID-19 Kenya
Watu waliopoteza maisha hadi sasa kote duniani kutokana na virusi vya corona ikiwa imevuka 20,000 huku zaidi ya watu nusu milioni kote duniani wakiambukizwa virusi hivyo hatari nchini Kenya kama zilivyo nchi nyingine, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanaendelea. Katika makala ya leo, mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi anaangazia tahadhari ambazo watu wa Kenya wanazichukua kujikinga na virusi vya corona na changamoto wanazokumbana nazo.
Ramani mpya ya WFP yadhihirisha athari za COVID-19 katika mlo shuleni
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limezindua ramani mpya ya kidijitali inayodhihirisha athari za virusi vya Corona, COVID-19 katika program zake za mlo mashuleni.
Vifo kutokana na COVID-19 duniani sasa 21,031, OCHA yahofia kwenye mizozo na majanga
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA leo imezungumzia hofu yake jinsi majanga na mizozo inavyoendelea kuwa kikwazo katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 huko Syria, Libya na Afghanistan huku ikipongeza hatua zilizochukuliwa na Sudan katika kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.