Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Ni bora kuzingatia ushauri wa kitabibu katika vita dhidi ya COVID-19: wananchi
Wakati huu ambapo dunia inapambana na janga la viruso vya Corona, COVID-19 taarifa za jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo nazo zinatoka kila kona lakini ushauri wa shirika la afya duniani WHO ni kuzingatia ushauri wa kitabibu unaotolewa na vyombo husika likiwemo shirika la WHO, wizara za afya na wataalam wa afya.
Kila tone la maji ni muhimu kwa dunia hii-WMO
Mafuriko, mvua za kupindukia, ukame na kuyeyuka kwa barafu ni ishara kubwa ya mabadiliko ya tabianchi yanayohusisha maji limesema shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.
CCBRT yatoa mafunzo yakilenga watu wenye ulemavu
Nchini Tanzania mafunzo kuhusu virusi vya Corona na jinsi ya kukabiliana navyo ambayo yanatolewa kwa watendaji wenye ulemavu katika hospitali ya CCBRT yemekuwa na manufaa makubwa wakati huu ambapo tayari taifa hilo la Afrika Mashariki limethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi hivyo. Ni kwa vipi basi? Tuungane na Hilda Phoya mwanafunzi anayefanya mafunzo kwa vitendo katika kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam ambaye amevinjari katika hospitali hiyo.
(Taarifa ya Hilda Phoya)
Tuweke silaha chini na tupambane na adui mkubwa COVID-19:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametoa wito wa kusitisha mapigano haraka kote duniani na nguvu zote kuzielekeza katika adui mkubwa wa sasa ambaye ni virusi vya Corona, COVID-19.
Uganda yachukua hatua zaidi kuzuia kusambaa kwa COVID-19
Serikali ya Uganda imeamua kufunga mipaka yake yote kwa abiria na kutangaza kuwa ni vyombo vyenye shehena za mizigo pekee ndio vitakavyovuka mipaka na kuingia nchini humo kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona au COVID-19 nchini humo mwishoni mwa wiki. Maelezo zaidi na mwandishi wetu, John Kibego kutoka Kampala.
(Taarifa ya John Kibego)
Hatua hii imetangazwa katika hotuba ya Rasisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa taifa baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona aina ya COVID-19 kuthibitishwa humo ncjhini.
23 Machi 2020
Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.
JINGLE (04”)
ASSUMPTA:Ni jumatatu ya Machi Ishirini na tatu mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI
Wafanyakazi wenye ulemavu CCBRT Tanzania wapatiwa mafunzo ya dhidi ya COVID-19
Nchini Tanzania mafunzo kuhusu virusi vya Corona na jinsi ya kukabiliana navyo ambayo yanatolewa kwa watendaji wenye ulemavu katika hospitali ya CCBRT yemekuwa na manufaa makubwa wakati huu ambapo tayari taifa hilo la Afrika Mashariki limethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi hivyo. Ni kwa vipi basi? Tuungane na Hilda Phoya mwanafunzi anayefanya mafunzo kwa vitendo katika kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam ambaye amevinjari katika hospitali hiyo.
Uganda yafunga mipaka yake kwa abiria juu ya COVID-19
Serikali ya Uganda imeamua kufunga mipaka yake yote kwa abiria na kutangaza kuwa ni vyombo vyenye shehena za mizigo pekee ndio vitakavyovuka mipaka na kuingia nchini humo kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona au COVID-19 nchini humo mwishoni mwa wiki.