Skip to main content

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.
Picha kwa hisani ya Yingshi Zhang

China yadhihirisha COVID-19 inaweza kudhibitiwa

Uzoefu wa China katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona unaweza kutumika kama somo kwa nchi zingine ambazo sasa zinakabiliwa na mlipuko huo wa COVID-19 amesema afisa wa shirika la afya ulimwenguni WHO nchini China.

World Bank/Arne Hoel

COVID-19 kuathiri elimu ya mamilioni ya watoto duniani kote

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema nchi 100 duniani zimefunga kabisa au kwa kiasi fulani shule na vituo vya elimu na kuwakoseha mamilioni ya watoto masomo, kwa sababu ya mlipuko wa COVID-19 unaoendelea. Grace Kaneiya na taarifa zaidi
(TAARIFA YA GRACE)
Shirika hilo sasa linasema hivi sasa linazisaidia nchi kusala suluhu ya jinsi ya Watoto kuweza kusoma wakiwa nje ya mazingira ya shule ikiwemo kupitia mtandaoni na nyenzo zingine za kidijitali

Sauti
2'37"