Pata habari kuhusu matumizi ya Akili Mnemba
Jinsi UNHCR inavyotumia AI kusaidia wakimbizi na kuboresha shughuli zake
Kwa kuwa duniani kuna takriban wakimbizi milioni 42 na shughuli za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) zinafanyika katika maeneo mbalimbali duniani, (UNHCR) hukusanya na kutumia kiasi kikubwa cha data kutoka vyanzo mbalimbali.
Fahamu programu ya JozaniAI, inayotumiwa Zanzibar kuboresha huduma za utalii
Programu ya JozaniAI, imeandaliwa kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambapo Naibu Mwakilishi wake, John Rutere akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya UN amesema tayari imeleta manufaa makubwa katika kutatua changamoto. Apu hiyo imepatiwa jina kutoka hifadhi pekee ya taifa visiwani humo, Jozani, iliyosheheni vivutio lukuki wakiwemo kima punju na misitu ya mikoko.
Kutoka Akili Mnemba (AI) hadi ‘roboti zinazoua: Guterres ataka mfumo wa kuisimamia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema ni lazima kuweko kwa udhibiti mpana wa kimataifa wa akili mnemba au (AI) wakati huu ambapo chipu za AI zenye uwezo mkubwa ambazo zilibuniwa kwa matumizi ya kiraia zinaanza kutumika vitani, ambako “roboti za kuua” tayari zinatumika.
Msukumo wa kimataifa wa usimamizi wa AI huku kukitolewa onyo la madhara ya janga
Je, akili mnemba (AI) inaweza kunufaisha wanadamu wote kwa njia salama, ya haki na bila kusababisha “madhara ya janga”? Hilo ndilo swali kuu linalojadiliwa katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa unaoanza leo Jumatatu huko Geneva, nchini Uswisi.
“Hatuwezi tena kusema hatukujua”: Guterres kuhusu ripoti ya AI
- Kisingizio cha ‘hatukujua’ sasa hakina mashiko
- Serikali zisisubiri kwani AI haisubiri
- Pengo la walio na AI na wasio na AI lizibwe
- Mashambulizi ya mtandaoni hayafahamu mipaka, hivyo ushirikiano wa kimataifa ndio jawabu
Akili mnemba (AI) - Faida, hasara na umuhimu wa usimamizi thabiti
Akili mnemba (AI) inaendelea kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi kuliko uwezo wa serikali kuandaa sera na kanuni zinazoendana nayo.
UNICEF yataka haki za watoto kuwa msingi wa utawala wa Akili Mnemba duniani
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limetoa wito kwa serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa katika utungaji wa sera na mifumo ya usimamizi wa Akili Mnemba, AI, huku likionya kuwa watoto wanatumia teknolojia hiyo kwa kasi inayozidi mara tatu ile ya watu wazima.
Janga la tabianchi: Mkuu wa UN aainisha mwelekeo wa kuhamia nishati jadidifu
Wakati wimbi la joto lililovunja rekodi likiendelea kuikumba Ulaya leo Jumanne, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa dhati wa kuchukuliwa hatua za pamoja na zenye matarajio makubwa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi yasiyodhibitiwa ili kuzuia uharibifu “usioweza kurekebishwa”.
Wakati AI Inabadili maisha ya mabilioni ya watu, inawapa kisogo wanawake: UN Women
- Mifumo mingi ya AI ina upendeleo dhidi ya wanawake.
- AI inaongeza ukatili wa wanawake mtandaoni.
- Wanawake ni wachache katika sekta za AI.
- Wanawake wako hatarini zaidi kupoteza ajira kutokana na AI.
- UN Women yataka usawa wa kijinsia uzingatiwe katika AI.
Guterres aonya kuhusu kuongezeka kwa kauli za chuki katika zama za kidijitali
Kauli za chuki zinaendelea kuwa tishio kubwa kwa mshikamano wa jamii na amani duniani, na mara nyingi ndiyo hatua ya kwanza kuelekea vitendo vya ukatili, migogoro na hata uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.