MKUTANO WA 75 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA74

Mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, #UNGA75 umefunguliwa Jumanne ya tarehe 15 mwezi Septemba mwaka 2020 kwenye makao makuu jijini New  York, Marekani. Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu utaanza Jumanne ya tarehe 22 mwezi Septemba mwaka 2020 na kumalizika tarehe 29 mwezi Septemba 2020. Katika ukurasa huu utapata taarifa motomoto kuhusu mjadala huo mkuu wa ngazi ya juu na matukio mengine ikiwemo miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Kwa kuwa mwaka huu Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 75, maadhimisho hayo yatafanyika kwa kuwa na siku moja ya mkutano wa ngazi ya juu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa 75 na siku hiyo ni Jumatatu ya tarehe 21 Septemba 2020. Tukio hilo maalum litakuwa na maudhui ya Mustakabali Tuutakao, UN Tuitakayo: Kusisitiza azma yetu ya pamoja ya ushirikiano wa kimataifa. Vikao vingine vya ngazi ya juu vitakavyofanyika wakati wa wiki za mwanzo za #UNGA75 ni mkutano wa ngazi ya juu kuhusu bayonuai, mkutano wa miaka 25 baada ya mkutano wa nne wa kimataifa wa Beijing, China wa mwezi Septemba 1995, Beijing +25.  UNGA75 inafanyika wakati wa janga la COVID-19 kwa hiyo vikao vitafanyika ukumbini lakini kwa kiasi kikubwa kimtandao ambapo wakuu wa nchi na serikali hotuba zao zitakuwa kwa njia ya mtandao.
 

1 Oktoba 2020

Hii leo mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unakuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kuchagiza utekelezaji wa usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake na mtoto wa kike, sambamba na maadhimisho ya miaka 25 tangu mkutano wa 4 wa kimataifa kuhusu wanawake uliofanyika Beijing nchini

Sauti -
13'32"

UNGA75 yafunga pazia, viongozi waahidi kudumisha ushirikiano wa kimataifa:PGA 

Wakati mjadala wa kihitoria wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia mtandaoni UNGA75 umefunga pazia leo, Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo amesema viongozi wa kisiasa wameahidi kuonesha mshikamano wa kimataifa.

Misaada ya kimkakati ni muhimu ili kukwamua nchi zilizotwama kutokana na COVID-19: Tanzania

Tanzania imezungumza kwenye mjadala mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuelezea msimamo wake katika masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa kimataifa, janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19, amani na usalama maziwa makuu na mustakabali wa Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo

Sauti -
2'59"

COVID-19 imetupa mafunzo-Uganda 

Tunauona ushirikiano wa kimataifa kama njia ya kushughulikia matishio magumu na mapya kama vile janga la COVID-19 ambalo limeathiri kila mwanachama wa jumuiya ya kimataifa, imeeleza sehemu ya kwanza ya hotuba ya Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo imesomwa kwa niaba yake na Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Uganda katika Umoja wa Mataifa, Balozi Philip Ochen Odida ikieleza pamoja na mengine, kile ambacho wamejifunza kutokana na ugonjwa huo. 

Tunashukuru kwa usaidizi dhidi ya COVID-19, sasa maisha yamerejea hali ya kawaida- Tanzania

Tanzania imezungumza kwenye mjadala mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuelezea msimamo wake katika masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa kimataifa, janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19, amani na usalama maziwa makuu na mustakabali wa Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo chombo hicho kinatimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake.
 

Tanzania tuna imani na UN, lakini ijitathmini nasi wanachama tujitathmini

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unafunga pazia leo Jumanne ambapo miongoni mwa nchi za Afrika zitakazohutubia ni Tanzania, ambayo imesema ujumbe wake mkuu kwenye jukwaa hilo ni kueleza kuwa bado ina imani kubwa na chombo hicho chenye wanachama 193.

Sauti -
2'18"

29 Septemba 2020

Tuna imani na UN, lakini ijitathmini nasi wanachama tujitathmini- Tanzania. Si haki kwa watu milioni 690 kulala njaa wakati chakula kinatupwa kila uchao yasema UN. Tunakufa kwa njaa. Tunahitaji chakula, Sudan Kusini walia baada ya mafuriko. 

Sauti -
13'45"

Tuna imani na UN, lakini ijitathmini nasi wanachama tujitathmini- Tanzania

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unafunga pazia leo Jumanne ambapo miongoni mwa nchi za Afrika zitakazohutubia ni Tanzania, ambayo imesema ujumbe wake mkuu kwenye jukwaa hilo ni kueleza kuwa bado ina imani kubwa na chombo hicho chenye wanachama 193. 
 

Nadia Murad ashutumu ukosefu wa nia ya kumaliza ukatili wa kijinsia unaotumika kama mbinu ya vita. 

Katika mazingira ambayo mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani kote ameathiriwa  na unyanyasaji wa kijinsia, uhalifu ambao unapaa zaidi kwa asilimia 200 katika mazingira ya mizozo, mshindi wa tuzo ya Nobel Nadia Murad amezishutumu serikali za ulimwengu kwa kushindwa kutoa rasilimali zinazohitajika kutengeneza mabadiliko ya kweli kwa jamii ambazo zimeathiriwa.   

Kama wazalishaji wakubwa wa chanjo tutahakikisha ya COVID-19 inamfikia kila mtu:India 

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Jumamosi Septemba 26 ameihakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba nchi yake ikiwa ni miongoni mwa wazlishaji wakubwa wa chanjo duniani, uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza chanjo utatumika ili kusaidia binadamu wote kupambana na janga la corona au COVID-19.