Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 4 wa Kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo

Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili kwa Maendeleo
30 Juni - 3 Julai, Sevilla, Hispania

Karibu kwenye matangazo maalum ya Habari za UN kuhusu Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ufadhili kwa Maendeleo (FFD4), unaofanyika Sevilla, Hispania.

Mkutano huu wa kihistoria unawakutanisha viongozi wa dunia, taasisi za kimataifa, sekta ya biashara, asasi za kiraia na mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto za dharura za kifedha zinazokwamisha maendeleo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

FFD4 unatoa fursa muhimu ya kubadili mazingira ya kifedha duniani na kuhamasisha rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya siku za usoni zenye usawa na endelevu zaidi.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa za moja kwa moja, maoni ya wataalamu, na taarifa za kina kutoka Sevilla.

UN News/Matt Wells

IOM yasema uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji ni muhimu

Katika Mkutano wa nne wa kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo. Anold Kayanda anaeleza zaidi.

Sauti
1'59"

02 JULAI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia wahamiaji na njia bunifu ya kuwawezesha kujikimu kimaisha, na malezi bora ya watoto nchini Tanzania. Makala tunasalia huko huko Tanzania kumulika uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya.

Sauti
9'59"
Waandishi wa habari wanafanya kazi katika kituo cha vyombo vya habari cha mkutano wa FFD4 huko Sevilla, Uhispania.
UN News/Matt Wells

IOM yataka uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji

Katika Mkutano wa nne wa kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) unaoendelea jijini Seville, Hispania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetoa wito wa kuimarisha uwekezaji wa kibunifu katika uhamiaji wa watu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kusaidia kuziba pengo la kila mwaka la dola trilioni 4 za ufadhili wa maendeleo.

Sauti
1'59"