Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 4 wa Kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo

Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili kwa Maendeleo
30 Juni - 3 Julai, Sevilla, Hispania

Karibu kwenye matangazo maalum ya Habari za UN kuhusu Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ufadhili kwa Maendeleo (FFD4), unaofanyika Sevilla, Hispania.

Mkutano huu wa kihistoria unawakutanisha viongozi wa dunia, taasisi za kimataifa, sekta ya biashara, asasi za kiraia na mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto za dharura za kifedha zinazokwamisha maendeleo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

FFD4 unatoa fursa muhimu ya kubadili mazingira ya kifedha duniani na kuhamasisha rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya siku za usoni zenye usawa na endelevu zaidi.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa za moja kwa moja, maoni ya wataalamu, na taarifa za kina kutoka Sevilla.

UN Photo/Manuel Elías

Guterres awaambia viongozi wa dunia huko Sevilla Ni wakati wa kufadhili mustakabali wetu na kubadilisha mwelekeo

Mkutano  wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa. Anold Kayanda amefuatilia na anatupasha zaidi

Sauti
2'45"

30 JUNI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 huko Sevilla Hispania, na siku ya Mabunge tukizungumza na mmoja wao kutoka Tanzania. Makala inatupeleka nchi Kenya na mashinani tunarejea huko huko Tanzania, kulikoni?

Sauti
11'41"
Sevilla ni mwenyeji wa mkutano wa nne wa Ufadhili kwa Maendeleo.
UN News/Matt Wells

Ni wakati wa kufadhili mustakabali wetu na kubadilisha mwelekeo, Guterres awaambia viongozi wa dunia huko Sevilla

“Tupo hapa Sevilla kubadilisha mwelekeo,” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia viongozi wa dunia Jumatatu, akiwaalika watumie fursa hii ya kipekee inayotokea mara moja kwa muongo mzima kuziba pengo la ufadhili la dola trilioni 4 linalozikabili nchi zinazoendelea ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu na kujenga dunia bora kwa wote.

Sauti
2'45"