
Karibu kwenye matangazo maalum ya Habari za UN kuhusu Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ufadhili kwa Maendeleo (FFD4), unaofanyika Sevilla, Hispania.
Mkutano huu wa kihistoria unawakutanisha viongozi wa dunia, taasisi za kimataifa, sekta ya biashara, asasi za kiraia na mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto za dharura za kifedha zinazokwamisha maendeleo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
FFD4 unatoa fursa muhimu ya kubadili mazingira ya kifedha duniani na kuhamasisha rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya siku za usoni zenye usawa na endelevu zaidi.
Endelea kuwa nasi kwa taarifa za moja kwa moja, maoni ya wataalamu, na taarifa za kina kutoka Sevilla.