Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa UNGA81

Mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa UNGA81

Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , UNGA81utafanyika kuanzia Jumanne, tarehe 22 Septemba hadi Jumamosi, tarehe 26 Septemba, na kufunga pazia  Jumatatu, tarehe 28 Septemba 2026.

Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu ni: “Kurejesha imani, kusimamia mabadiliko: Umoja wa Mataifa unaowahudumia wote.”

Mada kuu 6 zitajadiliwa na nchi wanachama

  1. Haki ya Maendeleo/Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs): Kuharakisha maendeleo ili kuhakikisha malengo ya mwaka 2030 yanaendelea kufikiwa, yakisisitizwa kupitia wakati wa SDGs, au SDG Moment.
  2. Haki na Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi na Mpito wa Haki: Kujadili malengo ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, mpito kuelekea nishati safi na kujenga uchumi unaozingatia mazingira.
  3. Kuongezeka kwa Kina cha Bahari: Kukabiliana na vitisho vinavyohatarisha uwepo wa mataifa ya pwani na visiwa.
  4. Amani na Usalama / Kutokomeza Silaha za Nyuklia: Kushughulikia migogoro ya kivita inayoendelea pamoja na changamoto za usalama duniani.
  5. Utayari wa Kukabiliana na Milipuko ya Magonjwa na Afya ya Dunia: Kuimarisha ushirikiano na mifumo ya kimataifa ya kukabiliana na majanga ya kiafya.
  6. Haki za binadamu na maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Durban kuhusu ubaguzi wa rangi.

MJADALA UNGA81: https://gadebate.un.org/en

UN News

“Maisha yanaweza kuwa mabaya kwa sababu ya vita, lakini tunaimba tu… na ninapoimba inanifanya kusahau matatizo yote na kuwa katika wakati huo." - Toussaint Chiza

Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa  kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao.

Sauti
9'37"

02 OKTOBA 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa  kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. 

Sauti
10'46"
Waandamanaji wakibeba mabango makubwa yaliyoandikwa "NUCLEAR BAN!" na "BAN THE BOMB WE WANT TO LIVE" wakati wa maandamano ya kupinga nyuklia katika Metropolitan Museum of Art huko New York.
© ICAN

UN: Wasiwasi waongezeka, mataifa yarudi kwenye ajenda ya kutokomeza silaha za nyuklia

Huku mvutano ukiendelea kushika kasi, athari za abadiliko ya tabianchi zikiongezeka na miundombinu ya nyuklia kushambuliwa katika nchi zilizokumbwa na vita za Iran na Ukraine, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa leo Jumanne zimerejea kwenye suala la msingi la upokonyaji wa silaha, zikihitimisha Wiki ya Mjadala wa Ngazi ya Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa wito wa kuimarisha zaidi mifumo ya ulinzi dhidi ya hatari za nyuklia.

Mwanamume aliyevaa suti ya kijivu na miwani akizungumza kwenye dawati la marumaru ya kijani katika ukumbi wa Mkutano Mkuu UN , huku mwanamke aliyevaa fulana nyekundu akifanya kazi kwenye kompyuta ya mkononi kando yake.
Picha ya UN/Loey Felipe

Mjadala Mkuu wa UNGA81 wafunga pazia

Baada ya siku sita za hotuba kutoka kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, neno moja lilijitokeza zaidi ya mengine yote: amani.

Ripoti hii ya mwisho ya Muhimu Yaliyojiri inakupatia muhtasari wa ujumbe ambao ulisikika kote katika Ukumbi wa Baraza Kuu, na inaangazia hatua ambazo chombo hicho chenye wanachama 193 kinapaswa kuchukua kuanzia hapa.