Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

UN News/Flora Nducha

Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania

Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza  Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kulinda

Sauti
4'26"