Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

UN Women/BrunoDemeocq

Bahari ni sehemu ya suluhisho la matatizo lukuki katika jamii - FAO

Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.

Bahari, ni makazi ya asilimia 80 ya majani ya wanyama, ambayo yanatumika kama chanzo muhimu cha wananchi kujipatia riziki na pia lishe kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.

Sauti
2'47"