Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
COP27 yafungua pazia, ni ukurasa mpya wa kufanya mambo tofauti :UNFCCC
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 umefungua pazia leo huko Sharm el-Sheik, Misri, na unapaswa kuuelekeza ulimwengu kwenye utekelezaji wa mipango iliyokubaliwa hapo awali ya kukabiliana na changamoto kubwa za ubinadamu, amesema wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Simon Stiell, katibu mtendaji mpya wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa (UNFCCC).
Ripoti mpya ya mabadiliko ya tabianchi ni historia ya zahma kubwa: UN
Ripoti mpya ya shirika la utabiri wa hali ya hewa la Umoja wa Mataifa WMO, iliyotolewa leo Jumapili, inaonyesha kuwa miaka minane iliyopita imekuwa ya joto zaidi katika historia ya rekodi, ikichochewa na kuongezeka kwa viwango vya gesi chafuzi.
Afya lazima iwe kitovu katika majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi COP27: WHO
Katika mkesha wa mazungumzo muhimu ya mabadiliko ya tabianchi COP27, yanayoanza kesho huko Sharm-el Sheikh nchini Misri, shirika la afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni WHO, limekumbusha kwamba mzozo wa mabadiliko ya tabianchi unaendelea kuwafanya watu kuwa wagonjwa na kuhatarisha maisha na kwamba afya lazima iwe msingi wa mazungumzo haya muhimu.