Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Rais wa Sudan asema deni la nje linairudisha nyuma nchi yake kufikia maendeleo
Deni la nje ni kikwazo kikubwa kinachozuia ukuaji wa kiuchumi na kijamii nchini Sudan na pia linazuia kutimiza malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs amesema leo Rais wa serikali ya mpito wa Sudan Abdel-Fattah AlBurhan Abdelrahman Al-Burhan wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha 77 jijini New York Marekani.
Amani inaimarika Sudan Kusini lakini bado tuna changamoto: Agany
Amani nchini Sudan Kusini inaendelea kuimarika huku idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wameanza kurejea katika makazi yao kwenye maeneo ambako utulivu umerejea na serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha mkataba wa amani unadumiswa amesema makamu wa Rais wa Sudan Kusini Hussein Abdelbagi Akol Agany akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza kuu hii leo mjini New York Marekani.
Vita ya Ukraine imetuletea adha dunia nzima: Azali Assoumani
Rais wa kisiwa cha Comoro Azali Assoumani akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha 77 amesema jumuiya ya kimataifa hivi sasa inakabiliwa na changamoto lukuki, kuanzia athari za kiafya kama janga la COVID-19 ambalo linaingia mwaka wa tatu ssasa, mabadiliko ya tabianchi hadi vita ya Ukraine ambayo imeleta adha kwa dunia nzima.