Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
07 Aprili 2022
Ungana na Leah Mushi anayekuletea jarida hii leo likianza na maadhimisho ya siku ya afya, WHO imetoa wito kwa serikali na wananchi kwa ujumla kutunza mazingira.
Leo pia ni siku ya kumbukizi ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya ya yalikuwa yanaweza kuzuilika.
pia utasikia kuhusu walinda amani wa Tanzania waliotembelea wafungwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Makala kutoka Zambia kuhusu ardhi oevu na ujumbe kwa watu kuendesha baiskeli kwa ajili ya kulinda afya zao.
Karibu usikilize.
Mabadiliko yanahitajika ili kulinda afya ya sayari ambayo afya ya binadamu inategemea-WHO
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limetoa wito wa dharura wa hatua za haraka za viongozi na watu wote kuhifadhi na kulinda afya na kupunguza janga la mabadiliko ya tabianchi kama sehemu ya kampeni ya "Sayari yetu, afya yetu" kuadhimisha siku ya afya, ambayo inafanyika wakati kukishuhudiwa mzozo mkubwa na udhaifu.