Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Jarida 12 Oktoba 2021

Karibu usikilize jarida linaloletwa kwako na Assumpta Massoi ambapo miongoni mwa utakayo sikia ni pamoja na wakulima nchini Kenya wanufaika na mradi wa viazi lishe chini ya ufadhili wa WFP. 

Binti Raba Hakim mkimbizi kutoka Ethiopia aanza masomo ya chuo kikuu kwa ufadhili wa Mastercard Foundation, na nchini Niger wakulima wapewa mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Pia utasikia makala na sauti kutokana mashinani.

Sauti
11'32"
©FAO/Giulio Napolitano

Wakulima Niger wapata mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Nchini Niger, mradi wa Benki ya Dunia wa hatua za kijamii za kuchukua hatua kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi, PACRC umesaidia jamii kuweza kutumia mbinu mpya mbunifu na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
(Taarifa ya Anold Kayanda)

Katika taifa la Niger ambalo ni moja ya mataifa yaliyoko ukanda wa Sahel, tishio la athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri. Viwango vya joto ni mara 1.5 kuliko kwenya maeneo mengine ya dunia.