Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Jarida Septemba 01 2021

Katika jarida na Grace Kaneiya hii leo utasikia ziara maalum ya Balozi Liberata Mulamula amaye ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania nchi Marekani kuzungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. 

Pia utasikia taarifa inayoangazia ripoti mpya ya hali ya hewa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO 

Sauti
12'46"