Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mnufaika mwingine kutoka West Guji, akishikilia mbuzi aliowanunua akitumia msaada w apesa taslim. Picha: IOM Ethiopia
Picha: IOM Ethiopia

Ruzuku za IFAD zatunusuru na maambukizi ya COVID-19

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo -IFAD umewawezesha wanakijiji nchini Ethiopia kujipatia kipato kupitia mradi wa uchimbaji wa mifereji ya kuzuia maji yasiharibu mazingira na kudhibiti mmonyomoko wa udongo uliokuwa ukiathiri kilimo na hivyo kuwakosesha mapato. Mradi huo pia umewawezesha kujinusuru na maambukizi ya corona.

Sauti
2'23"