Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

UN

Wakati ni sasa kuchukua hatua kukomesha uchafuzi wa hewa:Guterres

Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu, ni wakati wakubadili hilo sasa Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya hewa chafu inayovutwa na watu 9 kati ya 10 kila uchao duniani kote. Assumpta Massoi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Kupitia ujumbe wake wa maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya blu, Guterres ameonya kwamba hewa chafu inayovutwa inachangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya moyo, kiharusi,

Sauti
2'27"

07 SEPTEMBA 2020

Katika Jarida la Habnari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katika maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya rangi ya blu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka mshikamano kutokomeza uchafuzi wa hewa

-Nchini Pakistan mbinu za kupambana na ugonjwa wa Polio zawa mkombozi mkubwa katika vita dhidi ya corona au COVID-19 ikiwemo miundombinu yake

-Waalimu, wanafunzi na wazazi nchini Uganda waelezea changamoto za kusomea nyumbani wakati huu wa janga la corona au COVID-19

Sauti
12'51"