Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
COVID-19 imepunguza uchafuzi wa hewa lakini sio mbadala wa hatua za mabadiliko ya tabianchi:WMO
Kushuka kwa kiwango cha gesi chafuzi kunakohusiana na mlipuko wa janga la virusi vya corona au COVID-19 ni Habari njema za muda mfupi kwa mujibu wa mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.
Ni lazima tuilinde sayari dunia na watu wake-Guterres
Janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19 limefanya macho yote ya Dunia kuelekezwa kwenye mtihani huu mkubwa zaidi ambao ulimwengu umekumbana nao tangu Vita vya Pili vya Dunia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya mama sayari Dunia hii leo amesema
22 APRILI 2020
Leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea
-Umoja wa Mataifa unasema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kengele ya kuiamsha dunia kuchukua hatua kulinda sayari hiyo na watu wake hasa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya mama sayari dunia
- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na jiji la Nairobi wanachukua hatua kudhibiti kusambaa wa virusi vya corona au COVID-19, kwenye makazi dunia ya Kibera.