Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

14 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea 

-Dola milioni 477 zahitajika ili kunusuru maisha ya takriban watu laki tisa nchini Sudan kwa mahitaji ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lililozindua ombi hilo leo mjini Khartoum 

-Ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa kushirikiana na Benki ya dunia pamoja na wadau wenyeji, wanafanya juhudi za kuboresha huduma mijini pamoja na nishati ya umeme kwa mamilioni ya watu wa Yemen.

Sauti
10'41"