Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Baadhi ya wakulima nchini Malawi wameanza kulima nyanya katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
UNDP Malawi

Wakati ni sasa kila nchi kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema wakati wa kuchapuza kuchukua hatua zinazohitajika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya taifa ni sasa. Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo mjini New York Marekani kuhusu mkutano wa ngazi ya juu dhidi ya mabadiliko ya utakaofanyika wiki ijayo Bi. Mohammed amesema “Tunahitaji kusukuma mbele safari yetu kwa kutumia gia kubwa endapo tunataka kufikia malengo ambayo yamewekwa bayana na sayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu SDGs.”

Kituo cha kawi kutokana na nishati ya jua.
World Bank/Dana Smillie

Mabadiliko ya tabianchi

Umoja wa Mataifa unajitayarisha kwa ajili mkutano wa “Kuchukua Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Septemba mwaka wa 2019 huko New York, Marekani ambao ni moja ya mikutano ya ngazi ya juu ya tabianchi katika siku za karibuni, cha kujiuliza nihatua gani ambayo ulimwengu umepiga katika kukabiliana na shida ya tabianchi, na maendeleo hayo yanapimwaje?